Kuhusu Sayana Press
Sayana Press ni njia mbadala na rahisi wa kusawazisha homoni kwa mwanamke. Ni sindano yenye ncha nyembamba ambayo mwanamke anaweza kutumia kujiepusha na mimba kwa miezi mitatu. Mwanamke atatakiwa kuchoma sindano ya Sayana Press kila baada ya miezi mitatu jumla ya mara nne kwa mwaka mzima. Mwanamke anaweza kujichoma sindano ya dawa hii mwenyewe nyumbani au kwa msaaada wa rafiki au mtu yeyote wa familia. Tovuti hii inatoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia na kuna majibu na maswali mbalimbali yanayouliza mara kwa mara.
Sayana Press inazuia mimba tu. Kujikinga na magonjwa ya zinaa kama Ukimwi, tafadhali tumia kondomu za kike au za kiume kila ufanyapo mapenzi.
Kitu gani kinafanya Sayana Press kuwa tofauti?
Sayana Press ni njia ya uzazi wa mpango ya sindano inayoingia chini ya ngozi. Dawa inayoingia chini ya ngozi inaenda moja kwa moja kwenye safu ya ngozi wakati sindano nyingine huwa zinaishia kwenye misuli.
Sayana Press ina sindano ndogo na fupi kuliko sindano za kawaida, ndio maana wanawake wengi wametoa maoni yao kwamba ina maumivu kidogo au hakuna maumivu kabisa wakati wa kuchomwa sindano.
Sayana Press inakuja ikiwa tayari imeshajazwa dawa kwa hiyo inakuwa iko tayari kutumika.
Sindano hii ina vipande vinne:
Kopo dogo la mziringo.Kopo hili nilibeba hormoni za uzazi wa mpango;
Ukingo wa kopo ambao sindano imejishikiza;
Sindano ya hii dawa ni ndogo sana ( ina 3/8 urefu ndogo kuliko 1 cm );
Kitu za kufunikia sindano (Na pia huitwa ngao).
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Sayana Press:
Sayana Press inakuja kwenye mfuko mdogo wenye umbo la mstatili ambayo ni rahisi kuhifadhi, na inatakiwa ihifadhiwe mbali na watoto au wanyama. Sayana Press inapaswa kutumika maramoja tu, kama inavyoonyeshwa kwenye video, na inatupwa vizuri baada ya kutumika. Njia sahihi a kutupa Sayana press iliyokwisha tumika zinaelezewa kwenye sehemu ya maswali na majibu, lakini tafadhali ongea na mtu aliyekupa Sayana Press kuhusu njia nzuri za kutupa kwa usalama baada ya kutumia.
Maelezo zaidi kuhusu Sayana Press

Maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia Sayana Press: