Njia chache rahisi

Kutumia Sayana Press mwenyewe ni rahisi kujifunza. Hapo chini tunakupa hatua sita za kutumia Sayana Press.

Unaweza fanya yafuatayo mwenyewe nyumbani au unaweza omba rafiki au mtu yeyote wa famiia akusaidie. Itakavyokuwa, hizi hatua ni rahisi.

Tunapendekeza uangalie video kuongeza maarifa na pia kufuata maelekezo yafuatayo.


Kuangalia hii video ya kujifunza jinsi ya kuingiza Sayana Press

Hatua ya 1: Chagua na tayarisha sehemu ya kuchoma sindano

Chagua sehemu katika ngozi unapoweza kuchoma sindano- inaweza kuwa tumboni mbali na kitovu au kwenye mapaja kwa juu, zingatia isiwe sehemu zenye mifupa na sehemu ya ngozi yako yenye jeraha. Sehemu nyeupe kwenye picha inaonyesha sehemu unazoweza kujichoma Sayana press.

Yeyote atakayechoma sindano lazima awe amenawa mikono na sabuni kwa maji masafi na pia safisha sehemu ya ngozi utakayo tumia kuchoma sindano- inashauriwa zaidi kutumia pamba au nguo safi ambayo imelowekwa kwenye maji masafi au gozi iliyowekwa dawa. Kawa hauna dawa au sabuni, maji masafi yanatosha. Acha sehemu iliyosafishwa ikauke yenyewe kwa hewa (Usitumie taulo kukausha).

img-step-1

Hatua ya 2: Andaa dawa

Hakikisha mfuko wako wa dawa ya Sayana Press uko tayari, na haijaharibika. Ambalia mfuko wa dawa na hakikisha sindano ya Sayana Press haija expire na iko kwenye joto linalotakiwa.

Fungua mfuko wako wa Sayana Press na toa nje sindano. Angalia kwa makini kama mfuniko au ngao ya sindano kama iko sawa na kama kuna dawa yeyote iliyovuja kutoka kwenye kopo la dawa.

Kunatakiwa kuwe na nafasi kati ya ngao na ukingo. Kama hakuna ukingo wa sindano au nafasi, or kama kuna uharibifu wowote wa kopo la dawa, tupa kifaa hicho na tumia kingine.

img-step-2b

Hatua ya 3: Changanya dawa

Shika kifaa kwenye ukingo na tingisha vizuri kwa muda wa sekunde 30 mpaka upate rangi inyokaribia nyeupe and inayoacha weupe.

Kama kimiminika kilichopo kwenye kopo hakijichanganyi vizuri tupa kifaa hicho na tumia kingine.

img-step-3B

Hatua ya 4: Tayarisha sindano

Shika sindano kwa makini kwenye ukingo kwa mkono mmoja na shika ngao ya sindano mkono mwingine, kisha weka ngao sambamba na ukingo kuziba nafasi.

Utasikia sauti ikitoka sawa na sauti inayosikika unapokuwa unaziba kalamu na mfuniko. Ukishaziba nafasi, toa ngao ya sindano.

Sindano sasa imeshakuwa tayari na inatakiwa ishikwe ikiangalia juu ile dawa isimwagike.

img-step-4b

Hatua ya 5: Kuchoma dozi ya dawa

Kwa mkono mmoja, finya au vuta eneo la ngozi unapotaka kuchoma sindano ya Sayana Press. Na kwa mkono mwingine, shika ukingo wa sindano, kisha weka sindano kwenye sehemu ulipovuta ya ngozi kwa kwenda chini mkapa ukingo utakapo gusa ngozi kabisa.

Baada ya hapo, binya kopo ya dawa kwa kutumia kidole gumba na kidole kinachofuata. Binya taratibu kuacha dawa kuingia. Inapaswa kuchukua sekunde 5 mpaka 7. Unaweza kuona kimiminika kimebaki ndani ya kopo baada ya kuona kama imeisha ni kawaida.

Baada ya kumaliza kuchoma sindano ya dozi yote, toa sindano nje ya ngozi, na pia achia kujifinya. Unaweza binya sehemu uliyo choma sindano kwa kutumia pamba lakini usipapase au kufuta sehemu dawa ilipoingia.

img-step-5b

Hatua ya 6: Tupa Sayana Press

Weka Sayana Press kwenye chombo chochote chenye mfunikokama chupa iliyokwisha tumika yenye kichwa kipana na kifuniko.Weka mbali na watoto na wanyama,na usiruhusu mtu yeyote ashike sindano hizo.

Tupa container kama itakavyoelekezwa na muhudumu wa afya aliyekupa Sayana Press au fuata maelekezo ya kawaida wa jinsi ya kutupa vitu vyenye ncha kali au sindano zilizotumika.

img-step-6b

* Kama una wasiwasi au huna uhakika na jinsi ulivyotumia dawa hii, ongea na muhudumu wa afya aliye kupatia Sayana press. Usitumie sindano nyingine, lakini hakikisha unatumia njia nyingine za uzazi wa mpango mpaka muda wa kuchoma sindano nyingine wiki ya 12-14 (Miezi 3).
Maswali na Majibu

Kila kitu kuhusu Sayana Press.

Kwa maelezo zaidi kuhusu sindano ya Sayana Press