Kwenye kipengele hiki utapata majibu ya maswali yanayoulizwa sana kuhusu Sayana Press.

Bonyeza kwenye maswali kuona majibu.

  • Hakikisha hauna mimba kabla ya kutumia Sayana Press.
  • Unaweza kutumia Sayana Muda wowote ndani ya mwezi. Kama utaanza siku tano za kwanza mzunguko wa hedhi (Siku ya kwanza ni siku unayoanza kutokwa na damu), hapo Sayana press itaanza kufanya kazi papohapo.
  • Ukianza kutumia Sayana press muda mwingine wowote ndani ya mwezi hakikisha hauna mimba kabla ya kutoma sindano.Tumia njia nyingine za uzazi wa mpango kwa siku saba.Baada ya siku saba uko salama na Sayana Press.

Women who:
Wanawake ambao tayari wana mimba, anayesumbuliwa na shinikizo la damu, au ana historia ya mshtuko wa damu/kiharusi:

anayesumbuliwa mara kwa mara na kuumwa kichwa, aliye na uzoefu wa utokwaji wa dawa sehemu za siri ambazo hazijatibiwa, mwenye matatizo ya figo, mwenye kisukari kisichoweza kuthibitika, magonjwa ya sababiswayo na upungufu wa kinga mwilini, mtu anayedhaniwa kuwa na saratani la maziwa, mama anayenyonyesha mtoto ambae ni mdogo chii ya week 6.

Kama itatumika siku tano za mwanzo za mzunguko wa hedhi. (Siku ya kwanza unapoanza kutokwa na damu), baada ya hapo Sayana Press itanza kufanya kazi papo hapo.

Lakini kama itatumika siku nyingine kwenye mzunguko, inabidi uangalie kama una mimba kaba ya kutumia dawa na pia tumia njia nyingine mbadala ya uzazi wa paka kwa siku saba.

Baada ya siku saba uko salama na Sayana Press.

Ndio. Ni salama kubadili kutoka Depo-Provera na kutumia Sayana Press. Sayana Press ni dozi ndogo ya Depo-Provera na is nzuri kwa miezi mitatu.

Tumia ratiba sawa na uliyokuwa unatumia kwenye Depo-Provera.

Mara moja kila baada ya miezi mitatu (Wiki ya 12 au ya 14).

Unapaswa kuandika tarehe ulipochoma sindano ili uweze kukumbuka kirahisi.

Tunatoa maelezo haya kwenye kipengele ya jinsi ya kutumia na pia kwa kutumia video.

img-faq2
  • Sayana Press inabidi ichomwe kwenye tumbo au sehemu ya juu ya mapaja (Sehemu nyeupe kwenye picha). Kaa mbali na kitovu, jeraha au sehemu zenye mifupa.
  • Hakikisha unachoma sehemu mpya kila unapochoma.

Madhara ya Sayana Press yataisha wiki ya 15-52 baada ya sindano ya mwisho.

Yes. If you are not able to do it yourself, you can ask a friend or family member to inject you.
Before injecting, they should read this website, watch the video, and feel comfortable performing the steps.

Ndio, kama unashindwa kufanya mwenyewe unaweza kuomba rafiki au mtu yeyote ya familia akusaidie kuchoma.

Kabla ya sindano, unapaswa usome tovuti hii na kutazama video ili kuwa na ujasiri wa kufuata maelekezo yote.

Mifuko yote ya ziada ya Sayana Press yanapaswa ya hifadhiwe kwenye joto.

Usihifadhi Sayana Press kwenye friji, na weka mbali na moto, ikiwepo jua la moja kwa moja.

  1. Kwanza angalia tarehe ya kikomo cha matumizi. kama leo is tarehe baada ya siku ya kikomo cha matumizi, inabidi usitumie.
  2. Pili, angalia kimiminika ndani ya kopo wakat umefungua mfuko. Baada ya kutingisha, dawa inatakiwa iwe nyeupe au inayoelekea kuwa nyeupe.

Weka Sayana Press kwenye chombo chochote chenye mfunikokama chupa iliyokwisha tumika yenye kichwa kipana na kifuniko.

Usiruhusu mtu yeyote ashike sindano hizo.

Tupa container kama itakavyoelekezwa na muhudumu wa afya aliyekupa Sayana Press au fuata maelekezo ya kawaida wa jinsi ya kutupa vitu vyenye ncha kali au sindano zilizotumika.

Sayana Press ina ufanisi zaidi ya 99% ikitumika kikamilifu. Imebena hormone sawa na sindano za Depo Provera na inazuia mimba kwa miezi 3. Wanawake tu ambao hawana mimba ndio wataweza kuzuia mimba.

Tovuti ya Pfiber inatoa taarifa zaidi kuhusu Sayana Press, mwili wako unahitaji muda kuondoa homoni kwenye mfumo.

Baadhi ya wanawake wameweza kusumbuliwa na baadhi ya madhara ,unaweza kusoma kuhusu madhara hayo hapa: Madhara

Madhara mengi yanaweza kutatuliwa and mengine yanauwezekano wa kupotea miezi michache baada ya sindano ya mwisho.

Inategemea na ni muda gani umekuwa ukitumia Sayana Press, mwili wako unahitaji muda wa kuondoa hormoni kwenye mfumo wako wa mwili.

Wakati baadhi ya wanawake wanapata damu nzito kwenye mzungoko wao wa hedhi, wengi watapata damu nyepesi, wataona matone mepesi ya damu katikati ya mzunguko, au damu itakata kabisa bila kutoka. HMadhara haya yataisha pale utakapo acha kutumia Sayana Press.

Angalie kipengele cha madhara kwa maelezo zaidi.

Kila sindano inazuia yai la mwanamke kuachiwa kutoka kwenye ovary. Sayana Press haita hadhiri mimba ambayo tayari ipo.

Sayana Press haiwezi kusababisha mimba kutoaka na isitumike kwa ajili ya utoaji wa mimba.

Sayana Press inabeba 104 mg za depot medroxyprogesterone acetate, ambayo ni progestin.

Hii ni dozi ndogo ya homoni inayotumika kwenye aina nyingine ya dawa za uzazi wa mpango iitwayo Depo Provera.

  1. Kwanza hakikisha hauna mimba kwa kupima mimba.
  2. Kama huna mimba unaweza ukajichoma sindano inayofuata.
  3. Jaribu kutengeneza kumbukumbu ili usisahau siku nyingine.

Kiwango unachonunulia kinatofauti kwenye kila nch, Ila kama unaishi bara la Africa au Asia Sayana Press inapaswa ikugharimu 1$ – 2$ kwa dozi.

Mzunguko wako wa hedhi wa kawaida utarudi wiki ya 15 -52 (Miezi nne-Mwaka 1) baada ya sindano ya mwisho ya Sayana, nah ii inategemea ni kwa muda gani umekuwa ukitumia njia za uzazi wa mpango.

Zaidi ya 80% ya wanawake wanapata mimba ndani ya mwaka mmoja baada ya kuacha kutumia Sayana Press. Sayana Press hausababishi ugumba, kwa hiyo inabidi ufanye uchunguzi ni sababu gani nyingine inakusababisha usibate mimba baada ya mwaka mmoja.

Kama unanyonyesha,unaweza kuanza kutumia Sayana pale mtoto atakapo fikisha wiki 6 au zaidi. Sayana press haitazuia maziwa kutoka.

Kama haunyonyeshi, unaweza kutumia sayana siku 5 baada ya kujifungua. Mzunguko wako wa hedhi utakuwa mzito na mrefu kuliko kawaida kwa miezi kadhaa.

Zaidi na zaidi ya taasisi wanafanya kazi kuhakikisha Sayana Press inapatikana dunia nzima.

List kamili haipatikani lakini unaweka ukawasiliana nasi kwa email kwenye: easy@injectsayanapress.org tunaweza kukutaarifu ni wapi Sayana Press inapatikana kwenye nchi yako.

Ni kundi la watu ambao wamejitolea kuhakikisha huduma pamoja na taarifa zote za njia za uzazi wa mpaka zinapatikana. ifunze zaidi kuhusu sisi hapa.

Tafadhali tutumie email katika easy@injectsayanapress.org kutujulisha ni kitu gani kingine ungependa kukiona katiak tuvuti hii.

Pia unaweza kupitia rasilimali tulizotumia kujenga tovuti hii kwa maelezo zaidi.