Madhara yanayojitokeza mara kwa mara ni kama yafuatayo:
Mzunguko wa hedhi usio wa kawaida
Kuna wanawake wanapata hedhi isiyo ya kawaida, wanajikuta wamechafuka wakati wa mzunguko kwa damu ambayo ni nzito au nyepesi sana. Lakini madhara haya huisha baada ya mzunguko wa 2 au wa 3 wa sindano. Kwa wanawake wengi, hedhi husimama kabisa. Na hii ni kawaida kabisa na salama na haimaanishi kwamba una mimba. Unapoacha kutumia Sayana Press hedhi yako itarudi kama kawaida miezi michache baada ya sindano ya mwisho.
Mabadiliko ya Uzito
Kuna wanawake wametoa taarifa ya kuongezeka uzito au kupunguza uzito mpaka kilo 2.2 (paundi 5) wakati wanatumia Sayana Press. Kuhakikisha unakula vizuri na ubadili maisha na tabia itasaidia kupunguza mabadiliko ya uzito.
Kichwa kuuma
Baadhi ya wanawake wametoa taarifa za kuumwa na kichwa lakini unaweza kukitibu kichwa kama unavyotibu kichwa cha kawaida.Jaribu kutumia dawa za maumivu kama paracetamol, kula vizuri au kunywa maji zaidi kuona kama itasaidia.
Sehemu ulipochoma sindano
Unaweza unapata maumivu au ukahisi ulaini sehemu ulipochomwa sindano. Usikune sehemu ulipochoma sindano. Maumivu huondoka ndani ya siku moja au mbili.